Hatimaye, Kiernan Jarryd Forbes maarufu AKA aliyefariki kwa kupigwa risasi Februari 10, 2023 yanafanyika hii kifamilia huko Gauteng huku familia yake ikisema itaendelea kutoa kazi za Rapa huyo kama ilivyokuwa ikipaswa kufanyika akiwa hai.

Familia ya AKA ikiwa katika majonzi ya kuondokewa na mpendwa wao. Picha ya 24News.

Msafara wa marafiki, familia na wafuasi wa AKA wakiwa njiani kuelekea sehemu ya mwisho ya kumpumzisha rapa huyo na familia inasema wapo mbioni kuachia albamu yake ya ‘Mass Country’ April 24, 2023.

Hata hivyo, kutokana na mazishi hayo kuwa ni ya faragha, hakujawa na vielelezo vya msafara mzima ulipofika eneo la maziko wala matukio yaliyoendelea na kutokea.

Familia ya rapa huyo maarufu hapo jana ilifanya ibada ya kumuaga mpendwa wao huku ikiwaalika ndugu, jamaa na marafiki kushiriki na tayari wimbo mpya wa AKA umeachiwa usiku wa kuamkia leo Februari 18, 2023 ukijulikana kwa jina la ‘Company’ ambao amemshirikisha nyota wa Nigeria, KDO.

Dkt. Mwinyi afungua rasmi mradi wa maduka Darajani
Bilioni 6.2 za ujenzi wa Mabwawa kunufaisha Wafugaji nchini