Takribai Wanafunzi wa kike 480 wa Shule ya Sekondari Ngerengere ya Morogoro vijijini wamepatiwa msaada wa taulo za kike na chakula kutoka kampuni ya SOFTCARE ambayo inayojihusisha na utengenezaji na Usambazaji wa taulo hizo.

Akizungunza mara baada ya kutoa msaada huo, Meneja wa kampuni hiyo, Lucy Hubert Msami amesema Kwa mkoa wa Morogoro watazifikia Wilaya nne wakilenga kusaidia watoto wa kike kupunguza chamgamoto za kutohudhuria vipindi vya masomo.

Amesema, “Watoto wa kike Kwa mwezi Mmoja hukosa masomo Kwa Siku nne Hadi Tano kutokana na kukosa taulo za kike hivyo taulo Hizo zitasaidia zaidi ya miezi mwili na licha ya kutoa msaada katika shule hii pia tutazunguka katika shule zilizopo Wilaya za kilosa na Mvomero mkoani Morogoro.”

Mmoja wa wanafunzi waliopewa msaada wa taulo hizo, Amina Juma amesema shule yao inakabiliwa na changamoto ya kukosa chumba maalum cha kubadilisha taulo hali inayowalazimu kuacha vipindi vya masomo na kurudi nyumbani kujihifadhi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Rebecca Nsemwa ameipongeza kampuni ya SOFTCARE na kutoa wito Kwa wadau wengine kuiga mfano huo na kusema kwasasa serikali inajitahidi kujenga vyumba vya kibadilishia taulo ikiwemo shule hiyo ya sekondari Ngerengere.

Real Bamako yaapa kufa na Young Africans
Mbunge Dkt. Kimei ajivunia mafanikio Vunjo