Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Mussa Mbura amesema habari za kutokea kwa ajali ya Ndege inayodaiwa kutokea hii leo Februari 23, 2023 katika Ziwa Victoria Jijini Mwanza, si za kweli.

Mussa Mbura ameyasema hayo kwa njia ya simu na kueleza kuwa kilichokuwa kikifanyika ni mazoezi ya utayari ambayo yamekuwa yakifanyika mara kwa mara ili kuweza kujiandaa na utokeaji wa matukio ya dharua.

Amesema, “ni mazoezi ya kujiweka tayari tumekuwa tukiyafanya na miongozo inatutaka tuwe tunafanya mazoezi ya namna hii ili kuhakikisha utayari wetu pale inapotokea tatizo na yanatakiwa yafanyike kwenye Airport zote 58.”

Askari za Jeshi la Zimamoto katika mazoezi ya utayari.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Kiwanja cha Ndege Mwanza, Seneth Lyatuu amesema ajali hiyo ya mfano ya ndege katika Ziwa Victoria ni sehemu ya utekelezaji wa zoezi la utayari kama ambavfyo sheria imekuwa ikielekeza.

Hii leo Februari 23, 2023, kulizuka taarifa za ajali ya ndege ndogo iliyotokea katika Ziwa Victoria iliyokuwa ikiarifu kwamba vyombo vya uokoaji vikiongozwa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji vilikuwa vikiendela kwa ajili ya shughuli ya uokozi.

Aliyegongwa na Mwendokasi Kisutu yupo ICU
KMC FC yamkingia kifua David Kisu