Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga ameyataja mambo matano yanayoiangusha nchi ya Tanzania, na kusema yasipofanyiwa kazi nchi itakuwa kwenye matatizo, akianza na changamoto ya watu wengi kuwachukia watu wenye akili bila sababu na kutopenda kuambiwa ukweli, na kudai kuwa.

Kitwanga ameyasema hayo wakati akiongea na Waandishi wa Habari nyumbani kwake, na kulitaja jambo la pili kuwa ni wengi wa watu kutotaka mtu asaidie nchi kwa juhudi za kufanya kazi na humchukia kwakuwa baadhi yao hutaka washibe bila kufanya kazi.

Amesema, “mtu mwenye akili anachukiwa sijui ni kutokana na upeo wa mtu na kibaya zaidi mtu anayetaka kuisaidia chi kwa kufanya kazi hupigwa vita na hii inatokana na baadhi ya watu kutaka kushiba bila kutoa jasho, bila kufanya kazi.”

Mwanasiasa Charles Kitwanga.

Kitwanga ameongeza kuwa jambo la tatu ni watu kutopenda kuambiwa ukweli na kibaya zaidi msema kweli huonekana si lolote kwakuwa watu hawapendi kuona mambo yakisonga mbele, na kuanza kumchafua kwa vitu ambavyo si vya kweli.

Aidha, ameongeza kuwa jambo la nne ni mambo ambayo ni muhimu kuonekana hayana maana na kuyashabikia au kuyageuza kwa taswira tofauti, ili yasifanikiwe na hivyo kujikuta na wakati mgumu wa kushughulikia masuala ya kimaendeleo nchini.

Amelitaja jambo la tano kuwa ni watu kuyapa kipaumbele mambo mepesi, kujibu hoja zenye mashiko kwa kuzishusha hadhi na masuala magumu kuonekana hayana umuhimu akitolea mfano wa majibu yaliyotolewa Bungeni na mmoja wa Mawaziri kuwa mbunge asilete mambo ya waganga wa kienyeji.

Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

“Lile lilikuwa ni swali la kiuchumi na alitakiwa ajibu ‘fact’ yeye anajibu hovyo na huyo tunamwita ni mchumi lakini ni mchumi ambaye hajui uchumi, unapataje nguvu za kujibu hivi mbele ya Bunge, sasa nasubiri bajeti je waganga wa kienyeji watakubali kumsikiliza Waziri,” amefafanua Kitwanga.

Hata hivyo, amesema mtu mwenye ukweli na mwenye uwezo wa kufikiri mambo anapotaka kusema jambo ili kulisaidia Taifa ni vyema akasikilizwa na kuchukua ushauri wake, badala ya kuonekana kama ni adui kitu ambacho kinadumaza usongeshaji wa gurudumu la maendeleo kwa Taifa.

Jeshi la watu 24 kupambana Uganda
Hassan Dalali amng'ata sikio Mangungu