Aliyekuwa waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Charles Kitwanga amezungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu Rais John Magufuli alipotengua uteuzi wake kwa kosa la kuingia Bungeni akiwa amelewa.

Kitwanga ameeeleza kuwa alikuwa nchini Israel kwa ajili ya shughuli zake binafsi na kwamba amerejea nchini juzi akiwa na nguvu mpya kwa ajili ya kulitumikia taifa na jimbo lake la Misungwi.

Alisema kuwa amejipanga kurejea Bungeni wiki ijayo lakini kwanza atakutana na wananchi wa jimbo lake na kuzungumza nao ikiwa ni pamoja na kuwaeleza uhalisia wa kilichomsibu.

“Rais ni mtu mkubwa anaweza kufanya jambo lolote ili mradi havunji sheria. Hata akilichotokea kwangu ni Mamlaka yake halali, ingawa Mungu ndiye muweza wa yote. Mimi ni Mkristo safi, nasi tumefundishwa kusamehe saba mara sabini na kusahau yaliyopita,” Kitwanga anakaririwa na gazeti la Mtanzania.

Kitwanga alisema kuwa katika ziara yake jimboni kwake, hatakuwa na mlengo wa kutaka kuzua mabishano kutokana na kilichomsibu bali atawaeleza wananchi wake kile ambacho hata madiwani wake walikishuhudia kwani walikuwa naye mjini Dodoma kabla ya kupata taarifa za ‘kutumbuliwa’.

Mei 21 mwaka huu, Rais John Magufuli alitengua uteuzi wa Kitwanga aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo nafasi yake imechukuliwa na Mwigulu Nchemba.

Giuseppe Marotta: Hatujapokea Ofa Yoyote
Korea kaskizini kuichokoza Korea kusini tena