Mahakama ya Tanzania, imefanikiwa kupunguza Mlundikano wa mashauri kutoka asilimia 11 kwa mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 6 mwezi Desemba 2022.
Hayo yamebainishwa na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Wilbert Chuma wakati akizungumza kwenye kikao cha mapitio ya bajeti ya nusu ya mwaka 2022/23 na uchambuzi wa bajeti ya 2023/24, jijini Dodoma.
Amesema, hiyo ni hatua kubwa kwa Mahakama ambayo haijawahi ikitokana na usimamizi wa vikao vya kusukuma mashauri na mikakati usikilizaji mashauri huku akiwataka Watumishi kutoridhika na mafanikio waliyopata, bali wapambane zaidi ili kuzuia kabisa mlundikano wa mashauri.
Aidha, Chuma ameongeza kuwa, utekelezaji wa majukumu ya utoaji haki kwa wananchi uhakikishwe unaacha alama ya kukumbukwa kutokana na utendaji wao wa kazi kwa vizazi vijavyo ndani ya muhimili wa Mahakama.