Mahakama ya Tanzania, imefanikiwa kupunguza Mlundikano wa mashauri kutoka asilimia 11 kwa mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 6 mwezi Desemba 2022.

Hayo yamebainishwa na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Wilbert Chuma wakati akizungumza kwenye kikao cha mapitio ya bajeti ya nusu ya mwaka 2022/23 na uchambuzi wa bajeti ya 2023/24, jijini Dodoma.

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Wilbert Chuma akitoa maagizo kwa wajumbe kutoka mikoa na Kanda mbalimbali za Mahakama Kuu ya Tanzania wakati kikao cha mapitio ya bajeti ya nusu ya mwaka 2022/23 na uchambuzi wa bajeti ya 2023/24 kinachofanyika jijini Dodoma.

Amesema,  hiyo ni hatua kubwa kwa Mahakama ambayo haijawahi ikitokana na usimamizi wa vikao vya kusukuma mashauri na mikakati usikilizaji mashauri huku akiwataka Watumishi kutoridhika na mafanikio waliyopata, bali wapambane zaidi ili  kuzuia kabisa mlundikano wa mashauri.

Aidha, Chuma ameongeza kuwa, utekelezaji wa majukumu ya utoaji haki kwa wananchi uhakikishwe unaacha alama ya  kukumbukwa kutokana na utendaji wao wa kazi kwa vizazi vijavyo ndani ya muhimili wa Mahakama.

Mazao ya kimkakati kumaliza tatizo mafuta ya kula
Elimu ya mafunzo na ufundi stadi: Majaliwa aipongeza GGML