Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewapongeza wananchi kushiriki katika mikutano ya vyama vya siasa inayoendelea bila ya uvunjifu wa amani na kuwahimiza wazungumzaji wa mikutano hiyo kuhubiri amani, utulivu, mshikamano na maridhiano.

Dk. Mwinyi ameyasema hayo hii leo Februari 28, 2023 wakati akiongea na vyombo vya Habari na kuongeza kuwa, demokrasia inataka kushauriana na kueleza mambo ya kujenga si kuzusha au kusema mambo yasiyo na uhalisia ili kuupotosha umma.

Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

Akizungumzia changamoto ya Bandari ya Malindi, Dkt. Mwinyi amesema inasababishwa na uwepo wa gati moja dogo la kushushia mizigo ambalo linasababisha foleni za meli kushusha hadi siku saba.

Hata hivyo, amesema utatuzi wa changamoto hiyo ni kuwa na bandari kubwa zaidi na gati nyingi zenye vifaa vya kisasa, na kwamba Serikali imechukua hatua ya kuagiza zana mpya ambazo tayari zimeanza kutumika, ili kupunguza muda wa ushushaji mizigo bandarini.

Uchaguzi Nigeria: Waangalizi EU wakosoa utendaji wa INEC
Ushirikiano huleta ufanisi wa kazi: Dkt. Yonazi