Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amewataka Wakuu wa Wilaya kushirikiana na Viongozi wa Kata kuunda kamati za ulinzi, ili kulinda mali za wanufaika wa TASAF kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini.

Chalamila ameyasema hayo wakati alipotembelea na kukagua miradi na nyumba zilizowezeshwa kupitia mpango huo wa TASAF katika kata ya Karabagaine na Ijuganyondoza mkoani humo na kukemea tabia ya wizi inayofanywa na vijana kiasi cha kubomoa maadili ya Taifa.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila.

Amesema ‘’watu kama hawa wanaonufaika na tasaf tulinde mifugo yao na mali zao kwa kukemea tabia ya wizi inayofanywa na vijana tunaowalea wenyewe bila kufata misingi na maadili, mkuu wa wilaya pamoja na wenyeviti wote ni vikao vya mara kwa mara kuhusu ulinzi wa wanufaika hawa pamoja na mali za wengine ambao sio wanufaika na TASAF’’

Awali, akiwasilisha taarifa kwa Mkuu wa Mkoa Mratibu wa TASAF Manisapa ya Bukoba, Japhet Kanoni alieleza kuwa mbali na kaya hizo kuanzisha biashara, pia zipo ambazo zimeanzisha ufugaji na ujenzi wa nyumba za kuishi.

Pato ghafi la Taifa: GGML yamtaja Rais Samia
Mwili wa Bobby wasafirishwa Shinyanga