Mwili wa aliyekuwa beki wa timu ya Mtibwa Sugar Iddy Mobby umesafirishwa leo kuelekea Ngokolo mjini Shinyanga kwa ajili ya mazishi.

Beki huyo alifariki dunia jana Jumapili, Machi 5, 2023 katika Hospitali ya Benjamini Mkapa mkoani Dodoma wakati akipatiwa matibabu.

Mwili wa Mobby ukitolewa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo saa 5.30 asubuhi na kupakiwa katika basi la timu hiyo kwa ajili ya safari kuelekea Shinyanga.

Baadhi ya wachezaji wa Mtibwa Sugar walikuwepo wakiongozwa na Meneja wa timu hiyo, Henry Joseph na mke wa marehemu na mama mzazi.

Enzi za uhai wake Mobby aliwahi kuzitumikia Klabu za Polisi Tanzania, Mwadui FC, Stand United na Mtibwa Sugar ambayo ilimsajili mwanzoni mwa msimu huu 2022/23.

Kaya masikini kuwekewa ulinzi
Kapombe awahakikishia ushindi Simba SC