Serikali nchini kupitia Wizara ya Afya, imesema tafiti zimebaini kuwa takribani Watanzania 5,800 mpaka 8,500 wanahitaji huduma za kusafisha damu au kupandikizwa figo.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati katika Jengo la Wagonjwa wanaosafishwa figo lililopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

Amesema, “Kati ya waliopandikizwa figo Wagonjwa 103 wamepandikizwa nchini ambapo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imepandikiza wagonjwa 70 na Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma imepandikiza wagonjwa 335.”

Aidha, Waziri Ummy pia ameongeza kuwa hadi kufikia January 31, 2023 Wagonjwa 3,250 walikuwa wanapatiwa huduma ya kusafishwa damu na Wagonjwa 335 walikuwa tayari wamepandikizwa figo.

Rekodi mpya ujenzi wa Meli, itabeba Kontena 24,000
Ajali: Gari lagonga Treni Tabora