Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Ally Gugu amesema lengo na matarijio ya Mkoa nikuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa kuzingatia muda uliowekwa na viwango vya ubora unaotakiwa kwa kuzingatia thamani ya fedha.

Gugu ameyasema hayo wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika Wilaya ya Bahi kwa lengo la kukagua utekezaji wa miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo.

Amesema, watumishi wanaosimamia miradi hiyo wanatakiwa kuwajibika na kuhakikisha usimamizi madhubuti wa miradi yote ya maendeleo na kutoa angalizo juu ya hatua zitakazochukuliwa dhidi ya miradi ambayo haitakamika kwa wakati na ubora unaotakiwa.

“Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imeleta fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya afya na elimu katika Halmashauri zetu, tusiwe moja ya vikwazo katika kusimamia ukamilifu wa miradi hii, tunatoyaka kufanya yafanyike kwa wakati na hapa nisisitize kubwa zaidi kusiwe na viporo vya kutokamilika kwa miradi ya maendeleo.

Sote tudhamirie kukamilisha kazi zote zilizopangwa kutekelezwa katika mwaka huu wa fedha kwa kuzingatia mpango kazi,” Gugu alisisitiza, awali, Katibu Tawala Gugu alipata wasaa wa kuzungumza na Watumishi wa Wilaya ya Bahi na kuwataka kutumiza wajibu wao kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na
Kanuni za Utumishi wa Umma.

“Haki zinaenda sambamba na wajibu, hivyo timizeni wajibu wenu kikamilifu kila mmoja katika nafasi yake Halmashauri ya Wilaya ya Bahi iko katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa majengo 18 kati ya majengo 28 yanayotakiwa kwenye hospitali ya Wilaya ambapo jumla ya Shilingi Bilioni 4.3 zimetumika.

Kutokana na kukamilika kwa baadhi ya majengo katika Hospitali hiyo imewezesha kuanzishwa kwa huduma ya mionzi, huduma ya upasuaji ambapo mpaka sasa akina mama 212 wamefanyiwa upasuaji, uwepo wa huduma za X-Ray na Ultrasound na kutoa huduma kwa watoto waliozaliwa chini ya umri kamili wa mimba yaani Watoto njiti.

Mnamsaidia kazi au mnamsifia tu anaupiga mwingi: Mbunge CCM
Polisi waanza uchunguzi tukio la waumini kufunga ili wafe