Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Jaji George Masaju kuwa mshauri wa Rais masuala ya sheria.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus imeeleza kuwa uteuzi wa Jaji Masaju ambaye ni Jaji wa Mahakama Kanda ya Dodoma umeanza Aprili 20, 2023.

Jaji George Masaju.

Aidha, taarifa hiyo pia imeeleza kuwa Rais Samia amemteua Dkt. Richard Mayungi kuwa mshauri wa Rais, masuala ya Mabadiliko ya Tabia nchini na Mazingira.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Mayungi alikuwa Meneja wa Mazingira, katika Shirika la Umeme Tanzania – TANESCO na uteuzi huo umeanza rasmi Aprili 19, 2023.

Maambukizi ugonjwa wa Malaria yapungua nchini
Wengine 10 wa familia moja wauawa na watu wenye silaha