Jeshi la Polisi Mkoani Songwe, limesema mtu mmoja Meshack Mwambogolo amejinyonga katika msitu uliopo kitongoji cha Iyenga kilichopo Kijiji cha Shaji Kata ya Mlangali, baada ya mfanyabiashara mwenzake Joseph Muhume kutoroka na shilingi 118 Milioni za kununulia zao la Kahawa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya amesema mwili wa Mwambogolo umekutwa umening’inia kwenye mti hii leo Aprili 24, 2023 majira ya asubuhi, na kwamba marehemu aliacha ujumbe kuwa familia yake imsamehe kwa uamuzi aliochukua.

Amesema Mwambogolo ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Mlowo Wilayani Mbozi Mkoani Songwe, alitoa kiasi hicho cha pesa na kukiweka kwenye akaunti ya Muhume kwa ajili ya kununulia Kahawa alitoroka bada ya fedha hiyo kuingia kwenye akaunti yake.

“Mwambogolo kupewa taarifa kuwa Joseph ametoroka alichukua kamba na chupa ya sumu ya kuulia wadudu na kutoweka ndipo mwili wake ulikutwa asubuhi ukiwa unaning’inia kwenye mti.” alisema Kamanda Mallya na taratibu za kisheria ikiwemo kumpumzisha marehemu zinaendelea.

Robertinho aahidi kuishangaza Afrika
Ithibati kitabu cha Muungano imekamilika - Jafo