Serikali nchini kupitia Wizara ya Afya, inaangalia utaratibu wa kuona ni jinsi gani wanaweza kutenga fedha katika afua zinazolenga kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi – VVU kwa akina mama na watoto wachanga.

Mkuu wa Miradi wa Wizara ya Afya, Dkt. Catherine Joachim ameyasema hayo hii leo Mei 5, 2023 jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa, pia wanatarajia kutimiza azma hiyo kupitia vyuo vya mafunzo ambavyo huwapatia wakunga wa afya ujuzi unaolenga kudhibiti hali hiyo.

Amesema, “bado kuna kazi kubwa ambayo tunabidi tuifanye katika vituo vya afya, tunataka kuangalia ni jinsi gani tunaweza kutenga fedha kwa afua zinazolenga kupunguza maambukizi ya VVU kwa akina mama na watoto wachanga.”

Aidha, Dkt. Catherine ameongeza kuwa eneo jingine ni pamoja na suala la Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kuendelea kutoa huduma mkoba ili wale kuwahamasisha wanawake asilimia 15 ambao hawajifungulii vituoni.

Usajili wa Mayele Vipers SC wazua gumzo Uganda
Erik ten Hag aachwa njia panda Old Trafford