Ukuaji wa biashara kati ya Tanzania na Ufaransa umeongezeka kutoka kiasi cha shilingi billioni 27,784.8 kwa mwaka 2015 hadi bilioni 94,506.6 kwa mwaka 2022.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax amebainisha hayo wakati akifungua mkutano wa pili wa majadiliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Serikali ya Ufaransa Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax.

Mbali na kukua kwa biashara baina ya mataifa hayo mawili, pia kumekuwa na ongezeko la watalii kutoka Ufaransa ambapo kwa mwaka 2022 Tanzania ilipata watalii 100,600 kutoka Ufaransa na kuifanya kuwa nchi ya pili kwa watalii wa kimataifa kuja Tanzania.

Naye Balozi wa Ufaransa nchini, Nabil Hajlaoui amesema kufanyika kwa mkutano huo wa pili wa majadiliano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Ufaransa ni uthibitisho kuwa Tanzania na Ufaransa
zimekuwa na ushirikiano mzuri na imara.

Balozi wa Ufaransa nchini, Nabil Hajlaoui.

“Tumekuwa tukikutana mara kwa mara na kujadili masuala ya kikanda na kimataifa ili kuimarisha maendeleo ya miradi baina ya nchi zetu mbili katika sekta mbalimbali hususan mabadiliko ya tabianchi, uwekezaji, utalii, uchumi wa buluu, usalama wa baharini, na tumefanikiwa kujadili masuala yote,” alisema.

Mkutano huo pia umehudhuriwa na Makatibu Wakuu na Manaibu makatibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, Kituo cha Taifa cha Uwekezaji (TIC) na Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA).

Namba zinavyoikataa Ihefu FC Ligi Kuu
Cesc Frabregas: Chelsea itarudi kwa kishindo