Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limesema zaidi ya chanjo milioni moja za polio zilizokusudiwa kutolewa kwa watoto nchini Sudan zimeharibiwa, huku mapigano kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha Jeshi la akiba RSF yaliozuka mwezi Aprili yakiendelea.

Naibu mkurugenzi wa Ofisi ya Mipango ya Dharura wa UNICEF, Hazel De Wet amesema vifaa kadhaa vya kuhifadhia chanjo na chanjo zenyewe vimeporwa, kuharibiwa na kuteketezwa huko Darfur Kusini.

UNICEF ilikuwa katikati ya kampeni mfululizo za utoaji chanjo ya polio nchini Sudan, ambazo zilikuwa zikitolewa kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo mwishoni mwa mwaka 2022.

UNICEF ni miongoni mwa mashirika kadhaa ya misaada ya kibinadamu yaliyoripoti uporaji wakati wa mzozo wa Sudan na baadhi ya wafanyakazi wake walidhurika na vita hivyo ama kutekwa wakati wakiendelea na uwajibikaji.

Arsena Wenger: Arsenal inanipa mashaka
Young Africans akili kubwa Kombe la Shirikisho