Suala la ukabila na udini, limetajwa kuhusika katika mgogoro wa kivita unaoendelea kati wa majenerali wawili wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan na makamu wake, Mohamed Hamdan Daglo, wa kikosi cha Rapid Support Forces (RSF).

Majenerali hao wanagombania madaraka na maslahi ya kiuchumi hususani umiliki wa mali asili za nchi hiyo iliyopo kaskazini mashariki mwa bara la Afrika.

Waatalamu wa masuala ya migogoro na baadhi ya wanaharakati wa muungano wa makundi ya kiraia nchini Sudan, ambao hawakutaka majina yao yatajwe wakihofia usalama wao, wamesema mgorogoro huo ambao ulizuka ghafla wiki mbili zilizopita una historia inayoonyesha kuwepo kwa misingi ya ukabila na udini.

Mkuu wa jeshi la Sudan Jenerali Abdel Fattah Burhan (kushoto), na Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo Picha ya AFP.

Aidha, Prof. Dan Rothbath wa shule ya utatuzi wa migogoro katika chuo kikuu cha George Mason hapa Marekani alisema kwa kawaida vipengele vya migogoro yenye misingi ya udini au ukabila huwa havihusishwi moja kwa moja kuwa ni chanzo cha mgogoro.

Naye mkurugenzi wa Kituo cha Orfalea cha Masomo ya Kimataifa kilichopo katika Chuo kikuu cha California tawi la Santa, Barbara profesa Mark Juergensmayer alisema “Kijuu juu inaonekana kama ni vita kati ya RSF na SAF wakati inajulikana uasili wa RSF unatokana na wanamgambo wa Janjaweed ambao wanashukiwa walihusika katika mauaji ya kikabila huko Darfur.”

Nabi: Nimewaona Marumo Gallants, tutashinda
Azam FC yaanza safari ya Mtwara