Jeshi la Polisi Nchini, limesema limeona mjadala katika mitandao ya kijamii ikuhusiana na kifo cha Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Nusura Hassan Abdallah kilichotokea Mkoani Kilimanjaro.

Akitoa taarifa hiyo hii leo Mei 6, 2023 Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, David Misime amesema taarifa hizo zimekuwa zikihusisha kifo hicho na ajali iliyotokea Jijini Dodoma aprili 26, 2023 ikimhusisha Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi (Afya) Dkt. Festo Dugange ambapo zinadaiwa zimetokana na kipigo kutoka kwa mpenzi wake.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, “Jeshi la Polisi Tanzania lingependa kutoa ufafanuzi kuwa, Polisi Mkoa wa Kilimanjaro baada ya kuona taarifa hizo na sababu zinazotolewa, wameanza uchunguzi kwa watu mbalimbali, Hospitalini alikotibiwa binti huyo ambapo amesema wanashirikisha Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali,Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka – DPP na wadau wengine wa haki jinai.

Aidha Jeshi hilo pia limetoa wito kwa mtu yeyote mwenye taarifa zilizosahihi na zenye ukweli asisite kutoa taarifa hizo ili kuharakisha uchunguzi wa tukio hilo.

Hata hivyo, Misime amesema Jeshi la Polisi Nchini linasisitiza kuwa Uchunguzi wa tukio hilo ukikamilika taarifa kamili ya kilichobainika kitatolewa kwa umma na kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Mei 7, 2023
UDOM yathibitisha kifo cha Mwanafunzi wake