Watu kumi wamefariki katika maporomoko ya ardhi baada ya mvua kubwa kunyesha huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, eneo ambalo lina mzozo wa mapigano kati ya vikundi vya waasi na majeshi ya Serikali.
Msimamizi wa eneo hilo, Edgard Kasombolene amethibitisha idadi ya vifo vya watu 10 viliyotangazwa na utawala wa jimbo la Kivu Kaskazini huku Kamanda wa polisi wa eneo la Lubero, Kanali Jean Habamungu akisema xoexi la kuwatafuta manusura linaendelea.
Maafa hayo mapya, yanafuatia mafuriko na maporomoko ya ardhi ambayo yaliliathiri eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika siku za hivi karibuni kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
Zaidi ya watu 400 wamepoteza maisha wiki iliyopita huko Kivu Kusini, ikiwa ni idadi rasmi iliyotangazwa na Serikali kutokana na mafuriko katika eneo la Kalehe lililoko katika jimbo hilo huku taarifa zikisema idadi hiyo ni ndogo kuliko uhalisia.