Shughuli za uwindaji wa Kitalii zinazofanywa katika Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu yanayosimamiwa na TAWA nchini, zina manufaa na mchango katika kukuza uchumi waTaifa na mwananchi mmoja mmoja hasa wale waishio pembezoni mwa mapori ya akiba na mapori tengefu.

Hayo yamebainishwa na Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Mabula Misungwi Nyanda katika Ofisi za Pori la Akiba Kizigo lililopo Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida wakati akiongea na Watumishi wa Pori hilo kwenye ziara yake ya kikazi Kanda ya Kati.

Amesema, Serikali kupitia TAWA imetoa jumla ya Tshs. Billioni 9.6 Kwa Halmashauri na Vijiji wanufaika wanaoishi pembezoni mwa Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu Nchini ikiwa ni fedha zitokanazo na asilimia 25 ya ada ya Wanyamapori waliowindwa pamoja na Utalii wa picha katika kipindi cha kuanzia Aprili 2022 Mpaka Desemba 2022.

Kamishna Mabula pia amewaagiza viongozi na Watumishi wa Kanda ya kati kuhakikisha Vitalu vyote vya Uwindaji wa Kitalii katika Pori la Akiba Kizigo vinapata wawekezaji. Ikizingatiwa kuwa Pori hilo lina jumla ya Vitalu vinne vya Uwindaji ambapo viwili kati ya vinne vimepata wawekezaji

Kuhusu Wanyamapori Wakali na Waharibifu, Mabula amesema mkazo wa Wizara na Taasisi (TAWA), ni kuhakikisha kuwa adha wanayoipata wananchi kutokana na Wanyamapori Wakali na Waharibifu inadhibitiwa.

Dkt. Mwinyi aishukuru Norway kwa kuiunga mkono Tanzania
TAQA yaahidi kujenga vituo 12 vya usambazaji gesi asilia