Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi amelishtumu jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kutofanikiwa kudhibiti vitendo vya kihalifu na kiusalama Mashariki mwa DRC.

Tshisekedi ametoa kauli hiyo katika siku ya kwanza ya ziara yake nchini Botswana, na kudai kuwa kikosi hicho kinashirikiana na waasi wa M23 na huenda kikaondoka nchini mwake kufikia mwisho wa mwezi Juni.

Wanajeshi wa EAC wanaopambana na makundi ya waasi mashariki ya DRC. Picha ya Ben Curtis/ AP

Amesema, “kazi ambayo kikosi hiki kilipewa haijatekelezwa kabisa, leo tumeona katika baadhi ya maeneo ushirikiano kati ya kikosi cha jumuiya na waasi wa M23 kinyume na ilivyopangwa kwenye makubaliano.“

Kauli yake inakuja siku moja baada ya mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya SADC nchini Namibia, ambako jumuiya hiyo inayozijumuisha DRC, Afrika Kusini, Angola, Tanzania, Namibia, Zambia, Msumbiji, Zimbabwe, imesema itatuma vikosi vyake Mashariki mwa DRC.

Mwakinyo ashindwa kuvumilia, avunja ukimya
Lionel Messi ambwaga Hamilton tuzo za Laureus