Mshambuliaji Lionel Messi, ametwaa tuzo ya mwanamichezo bora wa Dunia ya Laureus, katika hafla iliyofanyika jijini Paris, Ufaransa.

Hii ni mara ya pili kwa mshambuliaji huyo wa Paris Saint Germain kutwaa tuzo hiyo ambapo mwaka 2020 aliibeba kwa mara ya kwanza, akishindana na Lewis Hamilton.

Katika tuzo hizo Messi alitajwa kuchukua tuzo baada ya kuisaidia timu yake ya taifa ya Argentina kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia mwishoni mwa mwaka jana.

Mshambuliaji timu huyo aliisaidia yake kutwaa taji la Kombe la Dunia nchini Qatar huku akishinda tuzo ya mchezaji bora wa michuano.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo, Messi mwenye umri wa miaka 35, alisema amepokea tuzo hiyo kwa heshima kubwa kutokana na mchango wake katika soka.

“Hii ni heshima katika kwangu na kabumbu kwa ujumla, naamini hata wengine watafanya vizuri na kutunukiwa,” amesema

Amesema anawashukuru wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Argentina na wachezaji wa PSG kwani bila wao ansingepata mafanikio hayo.

Ameongeza kusema Anaushukuru kuwa uongozi wa taasisi ya Laureus kwa kuandaa tuzo hizona wanamichezo wote waliompigia kura.

Jeshi EAC limeshindwa kupambana na waasi - Tshisekedi
Waziri Mkuu azindua huduma upandikizaji uloto