Meneja wa kikosi cha Inter Milan Simone Inzaghi, amesisitiza bado wana kazi ya kufanya ili kutinga hatua ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, licha ya ushindi wa mabao 2-0 walioupata katika mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya AC Milan juzi Jumatano (Mei 10).
Inter waliwafunga wapinzani wao wa jiji la Milan, dakika ll za kwanza kupitia kwa Edin Dzeko na Henrikh Mkhitaryan na kuuweka mchezo huo mikononi mwao kwa urahisi katika kipindi cha kwanza.
Milan waliimarika baada ya mapumziko lakini watashukuru bado wanaweza kuwafikia mabingwa hao wa 2010 baada ya matokeo ya kutatanisha mbele ya wafuasi wao kwenye mechi ya ‘nyumbani’ ya sare.
Inzaghi aliiambia Amazon Prime Video: Tungeweza kufanya zaidi ya mabao hayo mawili, lakini mechi nzuri. Tayari tumnepitia raundi kadhaa, tunajua tuko mbele.
“Sasa kutakuwa na mkondo wa pili, tutakuwa na mashabiki wetu na tunajua wazi bado tutalazimika kufanya bidii ili kutimiza ndoto.
“Niliomba jana (juzi) kwa moyo na akili. Walifunika kila inchi ya uwanja na walioingia walitusaidia.
“Hivyo ndivyo maonyesho kama haya yanavyofanywa. Sasa ni sawa kuwa na furaha, lakini tunajua bado tuna kazi.”
Naye mmoja wa wafungaji wa mabao, Dzeko aliwaonya wachezaji wenzake kutokata tamaa kabla ya mechi ya mkondo wa pili itakayochezwa Jumanne ijayo.
Bosi wa Milan, Stefano Piolo, alikasirishwa na mbinu ya timu yake. Ameambia Amazon Prime Video: “Tutajaribu kufanya vizuri zaidi katika mchezo wa mkondo wa pili. Nadhani mechi ilienda vibaya kutokana na mtazamo wa kimbinu na kiakili.