Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, kimepinga kauli ya Makamu Mwenyekiti wake, Tundu Lissu kuhusu maridhiano ya chama chao na Serikali kwamba baadhi ya vipengele walivyoafikiana vina utata.

Kauli hiyo, imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje, John Mrema, akisema suala la kuachiana majimbo halipo kwenye mambo 12 waliyojadiliana na Serikali.

Amesema, “hakuna kitu kama hicho suala la kupewa wabunge halimo kwenye mazungumzo ya maridhiano kilichofanyika tulikuwa na mambo 12 katika maridhiano na serikali na jambo hilo halipo.”

Hatua ya pingamizi hilo, inatokana na ziara ya Lissu mjini Kibaigwa, Dodoma ambapo alisema, amesikia kuwa katika hayo maridhiano kuna ahadi ya kuachiana wabunge na kwamba wameambiwa pia watapewa majimbo na kuendesha siasa za nusu mkate.

Rulani Mokwena: Tunaijua nje ndani Wydad AC
Jordan Henderson: Tutaimarika zaidi 2023/24