Mmoja wa Wafanyabiashara maarufu wa soko la Kariakoo, Sinyaa Kimambo ‘Mama Bonge’ ameishutumu Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA, kuwafuata mpaka nyumbani kudai kodi huku alilalamikia akilalamikia utitiri wa kodi ikiwemo kero ya fedha za takataka.

Kimambo ameyasema hayo hii leo Mei 17, 2023 mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika kikao cha wafanyabiashara katika uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Amesema, “kero kubwa kwetu ni kodi ya takataka, anakuja mtu wa taka dukani unalipa shilingi 40,000 akitoka hapo anakuja kuniambia pesa ya taka za stoo hivi stoo inazalisha taka Mheshimiwa Waziri Mkuu? alihoji mama bonge.

Aidha aliongeza kuwa, “yani tunanyanyasika sana watu wa vipodozi tunakuwa kama mbwa, TRA wanakuja mpaka nyumbani, nyumbani kuna ofisi au tukadange? aliongeza Sinyaa ambaye ni mfanyabiashara wa vipodozi.

Young Africans yamvuruga Kocha Singida Big Stars
Mtaala mpya kuwawezesha wahitimu kujiajiri - Wizara