Raia nchini Sudan, wameomba usaidizi wa mataifa kutafuta suluhu ya mapigano kufuatia vifo watu 17 waliuawa na wengine 106 kujeruhiwa baada ya roketi kugonga soko kusini mwa mji mkuu Khartoum, jumatano ya Mei 31, 2023.
Wakiongea kwa nyakati tofauti, wamesema idadi kubwa zaidi ya watu waliouawa kwa kushambuliwa kwa makombora katika mji mkuu tangu mapigano kati ya jeshi la Sudan na Kikosi Maalum cha RSF kuanza Aprili 15, 2023.
Shambulio hilo limekuja huku mazungumzo yaliyokuwa yakisimamiwa na Marekani na Saudi Arabia kumaliza mzozo huo yakishindikana ambapo Jeshi la Serikali tayari limetangaza kusitisha maongezi na wanamgambo wa SRF.
Aidha, eneo la Mayo lilishuhudia kuwa na mashambulizi makali na ya umwagaji damu ambayo yalisababisha vifo vya watu 17 na zaidi ya 106 kujeruhiwa, huku Muungano wa Madaktari wa Sudan ukisema idadi ya vifo vya raia katika vita hivyo imefikia watu 883.