Waziri wa Nishati, Januari Makamba ametaja vipaumbele vya bajeti yake katika mwaka wa fedha 2023/2024 ikiwemo kutekeleza miradi mbalimbali ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji umeme.

Waziri Makamba amtaja vipaumbele hivyo Bungeni jijini Dodoma, wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 kama ifuatavyo katika eneo la pili ambalo ni usafirishaji na usambazaji wa Umeme.

  1. Miundombinu ya kusafirisha umeme imeongezeka na kufikia jumla ya urefu wa kilomita 6,363.27 sawa na ongezeko la asilimia 4.1 ikinganishwa na kilomita 6,111.27 zilizokuwepo hadi kufikia mwezi Mei, 2022;
  2. Miundombinu ya kusambaza umeme imeongezeka na kufikia kilomita 168,548.36 sawa na ongezeko la asilimia 9.5 ikilinganishwa na kilomita 153,988.49 zilizokuwepo hadi kufikia mwezi Mei, 2022;
  3. Mradi wa Kusafirisha Umeme kutoka JNHPP hadi Chalinze – kV 400 umefikia asilimia 93.5 ikilinganishwa na asilimia 44 mwaka 2021/22. Aidha, ujenzi wa kituo cha Kupoza Umeme cha Chalinze ambacho ni sehemu ya mradi huo umefikia asilimia 64 ikilinganishwa na asilimia 3.59 mwaka 2021/22.
  4. Mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na kituo cha kupoza umeme cha Nyakanazi umekamilika. Utekelezaji wa mradi huo ulikuwa asilimia 99 mwaka 2021/22.
  5. Utekelezaji wa mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 400 kutoka Singida – Arusha – Namanga umefikia asilimia 95 ikilinganishwa na asilimia 79.3 mwaka 2021/22.
  6. Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 220 kutoka Rusumo hadi Nyakanazi umekamilika, ambapo utekelezaji wake ulikuwa asilimia 79 mwaka 2021/22.
  7. Mradi wa Kuimarisha Gridi ya Taifa (National Grid Stabilization Project) umeendelea kutekelezwa kwa kuunganisha Mkoa wa Kigoma katika Gridi ya Taifa kupitia kituo cha Nyakanazi na kuunganisha Wilaya za Ngara na Biharamulo kwenye kituo cha Gridi ya Taifa Nyakanazi.
  8. Serikali kupitia TANESCO inatekeleza jumla ya miradi 48 ikijumuisha miradi 20 ya kuongeza uwezo wa miundombinu ya usafirishaji umeme, miradi 12 ya kuboresha mifumo ya uendeshaji wa Gridi ya Taifa na miradi 16 ya ukarabati wa miundombinu ya usafirishaji umeme.
  9. Ilisainiwa mikataba 26 baina ya Serikali na Wakandarasi yenye thamani ya shilingi trilioni 1.9 ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kuimarisha Gridi ya Taifa.
  10. Mradi wa Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 132 kutoka Tabora hadi Katavi umefikia asilimia 26.7. Wizara Ya Nishati 5 Utekelezaji Wa Vipaumbele Vya Mwaka 2022/23
  11. Serikali imetoa Shilingi bilioni 16.43 kwa ajili ya malipo ya fidia kwa wananchi 6,500 wanaopisha mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 400 kutoka Iringa hadi Sumbawanga kupitia Mbeya na Tunduma (TAZA) na Wananchi 4,750 tayari wamelipwa fidia zao.
  12. Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 220 kutoka Morogoro hadi Dodoma kwa ajili ya uendeshaji wa Treni ya Umeme (SGR Lot II) umefikia asilimia 98 ikilinganishwa na asilimia 88 mwaka 2021/22.
  13. Jumla ya wateja 4,319,258wameunganishiwa umeme hadi mwezi Aprili, 2023, ikiwa ni ongezeko la asilimia 12.4 ikilinganishwa na wateja 3,842,096 waliokuwepo mwezi Juni, 2022.
  14. Miradi mbalimbali ya usafirishaji umeme, ikiwa ni pamoja na Msongo wa kV 400 kutoka Nyakanazi hadi Kigoma na Tabora hadi Kigoma kupitia Urambo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

KMC FC yaifuata TZ Prisons Rukwa
Wawili Coastal Union kuikosa Azam FC