Uongozi wa KMC FC, umeweka wazi maandalizi yao kuelekea mchezo unaokuja wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prison unaotarajiwa kupigwa Juni 6, mwaka huu kwenye Dimba la Nelson Mandela, Rukwa.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala, amesema: “Tumeondoka na wachezaji 24 ambao tumefanya nao maandalizi kwa wiki moja tangu ligi iliposogezwa mbele, kila kitu kinakwenda vizuri, hali ya wachezaji ni nzuri, wana ari na morali, kila mmoja yupo tayari kwenda kupambana.

“Iwe jasho na damu, jasho litoke damu au maji, lazima tuhakikishe timu yetu inakwenda kufanya vizuri na kutoa nafasi tuliyopo.

“Kwenye mchezo huo tutawakosa wachezaji wanne ambao ni Matheo Antony, Ibrahim Ame, Frank Mkumbo na Hance Masudi ambao ni majeruhi, hivyo tutawakosa mechi zote mbili zilizobaki.”

KMC ipo nafasi ya 13 ikikusanya alama 29, wakati Prisons ni ya nane na alama zake 34, zote zimecheza mechi 28.

Rais Dkt. Mwinyi azindua kamati kuzuia udhalilishaji
Makamba ataja maeno 14 usafirishaji, usambazaji wa Umeme