Takriban Watoto wapatao 300, miongoni mwao wakiwamo wachanga wameokolewa kutoka kituo cha yatima cha Al-Mayqoma, kilicho katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum.

Matukio ya kuhuzunisha katika kituo hicho, yaligonga vichwa vya habari mwishoni mwa mwezi uliopita, wakati mapigano makali baina ya jeshi rasmi la serikali na wanamgambo wa RSF yakiendelea jirani na eneo linalokizunguka kituo hicho.

Vifo vya watoto, viliangazia adha wanayoyapitia raia wa Sudan tangu uhasama wa kivita uliozuka kati ya jeshi linaloongozwa na Jenerali Abdel-Fattah Burhan na wanamgambo wa RSF chini ya Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo, mwezi Aprili.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Juni 9, 2023
Mike Maignan kusaini mkataba mpya AC Milan