Klabu ya AC Milan ipo kwenye mpango wa kumuongezea mkataba Mlinda Lango wake, Mike Maignan ambapo dau la mshahara wake litapanda, Maignan anatarajiwa kuongeza mkataba mpya ambao utamuweka kikosini hapo mpaka mwaka 2028.

Kipa huyo anakuwa kwenye orodha ya wachezaji ambao wanaongezewa mkataba, baada ya Rafael Leao kusaini dili jipya hivi karibuni.

Maignan alisajiliwa na Milan akitokea Lille ambayo alitoka kuipa ubingwa wa Ligue 1 msimu wa 2020-21 na msimu uliopita wa 2021-22 akiipa Milan taji la Serie A.

Katika mkataba wake mpya kama atakubali dili hilo basi mshahara wake utapanda kutoka euro 2.8m mpaka euro 4m kwa mwaka.

Majadiliano ya dili hilo jipya tayari yameanza kati ya viongozi wa klabu na wawakilishi wa kipa huyo.

Watoto 300 waokolewa Khartoum vita ikiendelea
Mackenzie awasilisha ombi kesi yake isikilizwe kwa haki