Mhubiri tata wa Kenya, Paul Mackenzie amewasilisha ombi katika Mahakama ya shanzu la kutaka kuhakikishiwa kuwa kesi yake itasikilizwa kwa njia ya haki kutokana na matamshi ya waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki.

Mapema wiki hii, Waziri wa Usalama wa ndani nchini Kenya, Kithure Kindiki alisema kuwa mhubiri huyo atakaa gerezani maisha yake yote hata kama Mahakama itampata bila hatia.

Awali, Rais wa Kenya, William Ruto naye aliagiza kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa Mhubiri huyo ambaye aliwataka Wafuasi wake kufunga hadi kufa, ili waende mbinguni haraka na kupelekea kupoteza maisha yao.

Kufuatia agizo hilo, Maafisa Wakuu wa usalama wakiongozwa na IGP Japhet Koome na Mkuu wa Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mohamed Amin walijiunga na Timu ya wachunguzi katika eneo Shahola palipopatikana makaburi na zoezi la kufukua miili lilianza.

Mike Maignan kusaini mkataba mpya AC Milan
Raphinha: Sitaki kuondoka Camp Nou