Kiungo Mshambuliaji kutoka Brazil na FC Barcelona, Raphinha amesema mpango wake ni kuona anaendelea kusalia kwa muda mrefu ndani ya kikosi cha klabu hiyo.

Raphinha alitua FC Barcelona mwanzoni wa msimu wa 2022-23 akitokea Leeds United ya England.

Mbrazil huyo katika msimu wake wa kwanza ndani ya Barcelona akiwa chini ya Kocha Xavi Hernandez, amefanikiwa kufunga mabao 10 na asisti 12 akiwa nyuma ya staa wa timu hiyo, Robert Lewandowski.

Raphinha ameonesha ubora wake na kupata nafasi hasa alipoumia Ousmane Dembele ambaye alikuwa nje kwa muda mrefu.

Winga huyo amesema: “Ipo wazi kuwa nataka kusalia hapa tena kwa miaka mingi zaidi na kuwa bora ndani ya Barcelona.

Winga huyo msimu wake wa kwanza amefanikiwa kutwaa taji la La Liga na Spanish Super Cup, huku akicheza UEFA kwa mara ya kwanza.

Mackenzie awasilisha ombi kesi yake isikilizwe kwa haki
Ummy azindua Baraza jipya la Madaktari Tanganyika