Kiongozi wa Azimio la Umoja One – Kenya, na Mwenyekiti wa Chama cha ODM, Raila Odinga amemtaka Naibu Rais, Rigathi Gachagua kuthibitisha matamshi yake ya hadharani kuwa yeye ni mtoto wa MauMau.

Hatua ya Odinga imekuja bada ya Gachagua kusisitiza kuwa yeye ni mwana wa MauMau, kutoka vuguvugu la Mlima Kenya, lililosaidia Kenya kupata uhuru kutoka kwa serikali ya mkoloni.

Mkamu wa Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua (kushoto), akiwa na Kiongozi wa ODM, Raila Odinga.

Amesema, “ikiwa kweli wewe ni mtoto wa MauMau kama unavyodai, jitokeze uthibitishie Wakenya,
na kiongozi wa wengi bungeni, Kimani Ichungwa naye atoe thibitisho kama ni mwana wa MauMau.”

Maumau kutoka Mlima Kenya, lilikuwa ni ‘jeshi la askari’ kutoka jamii ya eneo la Kati lililojificha msituni kukabiliana na askari wa mabeberu wa Muingereza na kusaidia Kenya kuwa huru mwaka 1963.

Angel Di Maria kumguata Benzema, Ronaldo
Tano Ligi Kuu hatarini kucheza Play Off