Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Argentina Angel Di Maria, ambaye alikuwa anakipiga katika Juventus inayoshiriki Ligi Kuu Italia maarufu Serie A, anatimka ndani ya timu hiyo kama mchezaji huru.

Di Maria alisaini mkataba wa mwaka mmoja ndani na Juventus akitokea kwa mabingwa wa Ufaransa, PSG katika majira ya joto Juni, mwaka jana.

Lakini mchezaji huyo ametangaza kutimka klabuni hapo mara moja kama mchezaji huru na hadi sasa haijafahamika ataenda klabu gani.

Winga huyo amekua katika ubora mkubwa ndani ya Juventus licha ya timu hiyo kutofanya vizuri msimu huu katika michuano ambayo wameshiriki na klabu kadhaa zimeelezwa kumnyemelea mchezaji huyo.

Benfica ambayo ndio timu ya kwanza ya Angel Di Maria kucheza barani Ulaya baada ya kutoka Argentina ina matumaini ya kumrudisha mchezaji huyo katika viunga vya Uwanja wa Estadio da Luz.

Vyanzo mbalimbali pia vinaeleza huenda Di Maria akaungana na magwiji wengine kuelekea Saudi Arabia ambapo mastaa wengi sana wanakimbilia.

Kwani hivi karibuni Karim Benzema ameondoka ndani ya Real Madrid na kutimkia huko hivyo inawezekana na mchezaji huyo akaungana nao huko.

Hassan Maulid awaangukia mashabiki Mbeya City
Gachagua kama wewe ni Maumau lete ushahidi - Odinga