Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Musukuma amekanusha uvumi kuwa wabunge walipewa fedha ili kupitisha azimio la Bunge kuhusu pendekezo la mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai wa kuanzisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii na uendelezaji wa bandari nchini.
Musukuma ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodomaa na kuongeza kuwa wabunge ni nao ni wananchi na hawawezi kupitisha kitu ambacho hakina maslahi kwa Taifa.
Amesema, “mimi nilienda Dubai tulifanya ziara ya siku tisa kiukweli wao wameendelea kuliko sisi,sasa tumepata hii fursa tunaanza kuponda,tunaanza kutukana hii sio sawa na hao wanaotangaza mitandaoni walishiriki kufanya maovu huko nyuma.”
Aidha, Musukuma amewataka watanzania kuendelea kuunga mkono serikali yao na kudai kuwa ataendelea kupambana na wanaiponda serikali na kusambaza uzushi kwenye mitandao ya kijamii waliotengeza uongo uliozua taharuki kwa watanzania.