Mkuu wa BEnchi la Ufundi Singida Big Stars, Hans Pluijm amesema kumaliza ligi katika nafasi ya nne kwao ni mafanikio makubwa kutokana na uchanga wa timu yake kwenye kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kocha huyo kutoka nchini Uholanzi ameeleza kuwa haikuwa rahisi kwao kutokana na ushindani mkubwa uliokuwepo msimu huu ambao unamalizika leo huku Yanga akiwa bingwa.

“Tunapaswa kujivunia na kujipongeza kwa hiki ambacho tumekipata katika msimu wetu wa kwanza kwenye Ligi Kuu, tumemaliza nafasi ya nne lakini pia tumefika hatua ya nusu fainali ya kombe la FA, na kucheza fainali ya Kombe la Mapinduzi kizuri zaidi tumepata nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao,” amesema Pluijm.

Kocha huyo amesema hawapaswi kujiona wanyonge kwa kushindwa kubeba taji lolote msimu huu ispokuwa wanarudi kujipanga ili kufanya vizuri katika mashindano yote ambayo watashiriki.

Amesema mikakati yao ni kubeba ubingwa wa Ligi Kuu na kufika hatua ya makundi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.

Simulizi: Dah! kumbe mdogo wangu anatembea na mke wangu
Nyaraka za siri: Trump kupandishwa kizimbani Miami