Mbunge wa Kahama Mjini, Jumanne Kishimba amesema kuwa elimu ni kitu ambacho alikuwa akikipigania sana Bungeni na mpaka kwenda kwenye mjadala wa kupata mtaala mpya wa elimu ambao utaenda kuondoa mgogoro wa ajira uliopo.

Kishimba ameyasema hayo wakati akifanyiwa mahojiano na Dar24 Media ambapo ameeleza sababu za kuchangia bungeni na kutaka mtaala wa elimu ubadilishwe.

‘’Kwakweli katika kitu ambacho kilikuwa kinaniumza sana kishwa ni elimu maana mimi mwenyewe ninawatoto najua ile shida ambayo nimepata wanadegree wengine wana Masters yani unamuona mtu kabisa huyu kwa kazi yake, peke yake hawezi’’.

‘’Alifundishwa akasoma lakini ukimuangalia unaona kabisa kuna vitu vingi sana anakosa pamoja na kwamba ameenda muda mrefu darasabi ndio maana mara kwa mara bungeni tumekuwa tukivutana’’

Amesema kuwa ’’tunafanya mabadiliko lakini mimi rohoni bado nilipenda mtu afundishwe kutafuta pesa akiwa darasa la kwanza kwasababu mzungu yeye aliposema kwamba wewe usome ufuate utaratibu huu ilikuwa akuajiri wewe lakini sasa hivi hakuna ajira’’ amesema Kishimba.

Aidha ameongeza kuwa ‘’mtoto wadarasa la kwanza usipomfundisho kwamba kitu hiki huwa kinakuwa hivi akaju madhara yake yatakuwa nini? maana yake hata ukikataa, mtoto asubuhi akiamka anaomba hela ya biskuti anaomba hela ya soda je? ukimfundisha yeye kutafuta hela ya soda kutakuwa na ubaya gani na je akijua hela madhara yake huwa nini? madhara yake atakuwa tu mfanyabishara au atatunza hela kuliko sasa hivi kukataa kabisa asifundishwe mtoto hela lakini afundishwe kuomba hela na kula hela’’

Amesema kuwa, mfano wa Nchi ya Libya ambayo ilikuwa ni nchi tajiri kabla ya kuingia kwenye machafuko ambapo amesema kuwa nchi nyingine yenye utajiri ni Botswana na kusema kuwa raia wake wanachunga ngombe na ndiyo nchi yennye pesa nyingi.

‘’tusema ukweli baada ya Libya kucollaps nchi yenye pesa nyingi kabisa ni Botswana lakini raia wake wanachunga ngombe sisi huku tunavita na ngombe na Madaktari wetu Mainginia kutoka Zimbabwe, Zambia, Tanzania na Kenya wote wanafanya kazi Botswana lakini raia wao wanachunga ngombe na  hao wamewaajiri madaktari wetu sasa kama mtu anangombe 200 na anapata karibu milioni 3 kwa mwezi si ni kazi hiyo hela ni kitu cha muhimu sana’’.ameongeza Kishimba

Aidha amesema kuwa ‘’kuna eneo kule kwenye jimbo langu kuna kijiji  ambacho kinaniuliza kila siku corona inarudi lini maana kipindi shule zimefungwa walipata mazao mara tatu zaidi wanawaza labda corona inafaida maana baada shule kufungwa wakapata mazao mengi’’

Kishimba amesema kuwa elimu inafaida na hata maendeleo yalipo yameletwa na elimu na kusema kuwa elimu isiwe kitu cha kukalili.

“Kwanini mtu akalili kwanini unakariri kwamba nikijua hivi si ruhusiwi kikijua hiki kikawa hela ila unatakiwa kikijua ili ukafanye kazi kwa mtu yani nataka kwamba wakati watu wanasoma wakipata upenyo wa kujua kumbe hiki huwa hivi hao waende wakafanye hivyo ndio maana yangu mimi ili tuende kama wachina kuliko sasa hivi kila kitu mnajua lakini hamuwezi kitengeneza hela.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Juni 19, 2023
Jude Bellingham: Ninamkubali sana Zidane