Kabla ya kushuka dimbani kesho Alhamis (Juni 22) katika mchezo wa Mkondo wa Pili wa ‘Play Off’ dhidi ya Mashujaa FC, benchi la Ufundi la Mbeya City, limejigamba kuwa timu yao bado ina nafasi ya kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2023/24.

Mbeya City ilikubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Mashujaa FC katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano uliochezwa juzi Jumatatu (Juni 19) Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Kocha Msaidizi wa Mbeya City, Paul Nonga, amesema kikosi chake kitacheza pambano la marudiano katika uwanja wa nyumbani na anaamini kitapata matokeo mazuri yatakayowabakiza Ligi Kuu.

“Tumefanya makosa katika mechi ya awali na kupoteza lakini nafasi bado ipo na tutashinda kwa kishindo na kubaki katika mashindano, timu ipo vizuri na inaendelea kujipanga kuwakabili wapinzani wetu,” amesema

Mbeya City itatakiwa kushinda kuanzia mabao 2-0 katika mchezo wa marudiano wakati Mashujaa inahitaji ushindi wowote.

Ilkay Gundogan azitega Man City, FC Barcelona
Vurugu Gereza la Wanawake zauwa zaidi ya 40