Makubaliano kati Tanzania na Serikali ya Dubai juu ya ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji Kazi wa Bandari Tanzania, unalenga kuboresha uendeshaji wa shughuli za Bandari nchini kwa kuongeza tija na ufanisi, kusimika mifumo ya kisasa ya TEHAMA na kuwajengea uwezo kupitia mafunzo Watanzania katika uendeshaji wa shughuli za Bandari.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Sheria Wizara ya Ujenzi, Mohamed  Salum na kusema utaratibu huo wa makubaliano, unahusisha hatua kubwa tatu ambazo ni makubaliano baina ya Serikali na Serikali (Intergovernmental Agreement), makataba wa Nchi mwenyeji (Host Government Agreement) na mikataba mahususi ya utekelezaji wa huduma (Definitive Agreement-Concession or Service Level Agreement).

Mkurugenzi wa Sheria Wizara ya Ujenzi, Mohamed  Salum.

Amesema, “mkataba huu si mkataba wa kibiashara, na wala si mkataba unaotoa haki kwa DP World kuwekeza nchini, ni lazima Kampuni hiyo ije na itafanya majadiliano ya kuingia mikataba ya uwezekaji, na imewekwa wazi kuwa makubaliano yatafanyika kwa sheria za Tanzania na kusimamiwa na sheria za Mahakama zetu na umefanyika baina ya nchi na nchi ili yafanyike kwanza majadiliano ya uwekezaji.”

Bandari ya Dar es Salaam.

Aidha, ameongeza kuwa “mkataba huo umekusudia kuleta tija na ufanisi wa Bandari suala ambalo limekuwa changamoto kubwa kwa Serikali katika kufikia malengo ya kiuchumi na kijamii na haujatoa Bandari zote kwani sheria ya Bandari namba 17 ya mwaka 2004 (5), (12), kinaelekeza kuwa mamlaka ya kusimamia Bandari nchini yamekasimiwa kwa TPA na ndiyo yenye mamlaka ya kusema nini kifanyike.”

“Mkataba huu umeongelea suala la mapato yaani Kodi, Tozo na Ushuru kwenye ibara ya 18, kwamba utakusanywa kwa mujibu wa sheria zetu, lakini tutapata nini na anawekeza nini kwenye huu mradi, hapo ni lazima TPA sasa akae naye wajue atawekeza kiasi gani na atalipa kiasi gani, ingawa tunaamini tutapata sana kwasababu tunaamini kwenye tija na ufanisi na tutamuwekea masharti na mapato yatakuwa makubwa,” amefafanua Salum.

Mauaji: Watano familia moja wachinjwa, nyumba zateketezwa
Puuzeni, hakuna picha mabaki ya Nyambizi Titan: U.S.C - Guard