Klabu ya Manchester United inajipanga kutuma ofa rasmi ya kumsajili kiungo kutoka nchini Ecuador na klabu ya Brighton & Hove Albion Moises Caicedo.

Mwanzoni mwa juma hili klabu hiyo ya Jiji la Manchester ilifanya mawasiliano ya kwanza na Uongozi wa Brighton & Hove Albion ili  kuulizia huduma ya kiungo huyo.

United wamekuwa kwenye mawindo ya kiungo mpya wakati huu wa majira ya kiangazi, huku ofa yao ya Pauni milioni 55 kwenda klabu ya Chelsea kwa ajili ya kiungo Mason Mount ikigonga mwamba, lakini sasa wanaangalia uwezekano wa kumsajili Caecedo.

Lakini pia mashetani hao wekundu wanavutiwa na kiungo Adrien Rabiot wa Juventus, lakini kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo ya Italia.

Caicedo alikuwa kwenye kiwango bora akiwa na Brighton & Hove Albion msimu huu na mwezi Januari klabu hiyo ilikataa ofa ya pauni milioni 70 kutoka klabu ya Arsenal iliyokuwa ikiwania huduma ya kiungo huyo wa ulinzi.

Hii sio mara ya kwanza kwa United kuonesha kuvutiwa na kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 wakati akiwa bado anacheza klabu ya Independiente del Valle ya nchini kwao Ecuador kabla ya kujiunga na Brighton & Hove Albion.

Zitambue Nchi 11 hatari zaidi Duniani
Kocha Mashujaa FC afunguwa 2023/24