Kiungo kutoka nchini Gambia Gibril Sillah, amechimba mkwara mzito baada ya kuweka mazingira mazuri ya kutua Azam FC msimu ujao 2023/24, kwa kusema anakuja kuuwasha moto Bongo.

Uongozi wa Azam Juni 28, mwaka huu ulitangaza kufikia makubalino na Sillah ambaye anatarajiwa kutua nchini hivi karibuni kwa ajili ya kukamilisha taratibu zote za usajili na kuanza kuitumikia timu hiyo.

Sillah ambaye atajiunga na Azam FC akitokea klabu ya Raja Casablanca, msimu uliopita akicheza kwa mkopo kwenye kikosi cha JS Soualem kinachoshiriki Ligi Kuu ya Morocco, alihusika kwenye mabao 11 akifunga mabao saba na kutoa pasi za mabao nne.

Sillah amesema: “Natarajia kuja Tanzania hivi karibuni kwa ajili ya kukamilisha taratibu mbalimbali za usajili wangu, nafahamu Azam ni miongoni mwa timu zenye malengo makubwa msimu ujao.

“Hivyo niwatoe hofu mashabiki wa Azam kwa kuwaahidi kupambana na kushirikiana na wenzangu kuhakikisha tunafanya vizuri na kufikia malengo yetu, binafsi niko tayari kuanza kazi rasmi Tanzania.”

Wanasayansi Tanga waukataa ukatili, uzinzi
KMC FC yafyeka 11 usajili 2023/24