Uongozi wa Klabu ya Kagera Sugar umeripotiwa kuwa katika mazungumzo na Beki wa lhefu FC, Juma Said Nyosso ili kurudisha klabuni hapo msimu ujao 2023/24.

Beki huyo aliyewika na timu mbalimbali zikiwemo za Simba SC, Geita Gold na Mbeya City anahitajika tena kurudi kwenye timu hiyo ambayo awali aliwahi kuitumikia kwa mafanikio makubwa kati ya 2017 hadi 2020 alipoondoka na kwenda timu zingine.

Hatua hiyo ya Kagera Sugar, inajiri baada ya viongozi wa Ihefu kuonekana wazi kutokuwa na mipango na beki huyo wa zamani wa Ashanti United anayetumia nguvu na akili kuwathibiti washambuliaji wasumbufu.

Hata hivyo hadi sasa Ihefu FC haijaweka wazi kama itaendelea ama kumuacha Nyosso, ambaye msimu uliopita aliisaidia klabu hiyo ya mkoani Mbeya kufanya vizuri katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania.

Mpango wa kutaka kurejeshwa Kagera Sugar unadaiwa kusukwa na Kocha Mkuu wa kikosi cha timu hiyo Mecky Mexime ambaye amekuwa na uhusiano mzurina Juma Nyosso.

Moise Caicedo apanda thamani England
Sadio Mane ashikilia usajili wa Harry Kane