Mpango wa Manchester United kusajili Mshambuliaji mpya kwenye dirisha hili kubwa la usajili unaonekana kugonga mwamba, ambapo inaelezwa huenda Kocha Mkuu wa timu hiyo, Erick Ten Hag akalazimika kumrejesha tena, Marcus Rashford katikati msimu ujao.
Kusajili Mshambuliaji Mpya wa kati kulikusudiwa kuwa kipaumbele kikuu cha Manchester United kupitia dirisha hili la usajili, lakini hadi sasa wamekamilisha huku usajili wa kiungo Mason Mount pekee, huku wakiendelea kupigania saini ya kipa Ande Önana.
Licha ya juhudi kubwa za Marcus Rashford, United msimu uliopita walikusanya mabao 58 tu, katika mechi 38 za Ligi Kuu ya Uingereza, pungufu sana kuliko wapinzani wao waliowazunguka kwenye msimamo wa ligi.
Hata hivyo kwa mshangao wa wengi, United wamelenga maeneo mengine kwa ajili ya kuboresha hadi sasa majira ya joto.
Dili la Onana kutua United linakadiliwa kuwagharimu zaidi ya pauni 50m, hivyo kutokana na bajeti ya Ten Hag ambayo ni pauni 120m pekee suala la kusajili mshambuliaji mpya linaonekana kugonga mwamba kutokana na fedha zitakazosalia.
United wamehusishwa na nyota wa Uingereza Harry Kane ambaye Mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy amedai anahitaji zaidi ya pauni milioni 100.
Mkali wa Mabingwa wa Soka nchini Italia SSC Napoli, Victor Osimhen naye inaonekana kuwa ngumu kumpata kutokana na thamani yake sokoni kwa sasa.