Kocha Mauricio Pochettino, amesema wachezaji wake wa Chelsea wanahitaji kukua kama timu baada ya kuchapwa bao 1-0 na Aston Villa kwenye Uwanja wa Samford Bridge na hivyo kupoteza kwa mara ya tatu msimu huu.

Mchezo uligeuka baada ya kutolewa nje kwa Malo Gusto wa Chelsea baada ya dakika 58.

Lucas Digne alichezewa rafu kwenye kifundo cha mguu na baada ya ukaguzi wa VAR mwamuzi Jarred Gillett, alibadilisha kadi ya njano ya awali na kuwa nyekundu kwa mchezo hatari.

Pochettino alimuingiza Ben Chilwell na kumsogeza Axel Disasi kuwa beki wa kulia, lakini hakukuwa na matokeo chanya kwa Chelsea.

Ulikuwa uamuzi ambao uliwasumbua, kwani kwa upande wa wenyeji walijidhatiti na Moussa Diaby alimtengenezea pasi Ollie Watkins, ambaye alifunga bao.

Baada ya mchezo huo, Pochettino alisema wachezaji wake wanatakiwa kukua kama wachezaji na wanapaswa kuchukua hatua baada ya mwanzo mbaya wa timu msimu huu.

“Ni jukumu letu na jukumų la wachezaji.” alisema Pochettino.

“Hatuwezi kulaumu VAR au mwamuzi. Tunatakiwa tufanye tofauti kwa namna tofauti.

Sitalaumu wala kusema lolote dhidi ya Malo Gusto. Hali hutokea kwenye soka na huathiri mchezo na timu kwa njia hasi. “Tunahitaji kukua kama timu, si tu kwa njia ya kibinafsi.”

Ancelotti: Hatukuwa makini, mnilaumu mimi
Waziri Mkuu, Rais Samia waitwa Morogoro