Rais wa Marekani, Joe Biden, amekuwa Kiongozi Mkuu wa kwanza wa Marekani aliye madarakani kushiriki kwenye  mgomo wa wafanyakazi, wakati alipojiunga na Waandamanaji katika viunga vya jiji la Detroit.

Maandamano hayo, yanaingia katika wiki ya pili ya mgomo wao, wakitaka malipo zaidi, muda mfupi wa kufanya kazi na mahitaji mengine kutoka viwanda vikubwa vitatu vya kutengeneza magari.

Rais wa Marekani, Joe Biden alipokuwa akiongea wakati wa mgomo huo, katika mji wa Van Buren Michigan. Picha ya Evan Vucci/AP.

Wafanyakazi hao, pia wanataka nyongeza ya malipo kwa asilimia 40, kufanyakazi kwa saa 32 kwa wiki na zaidi wakigusia namna kampuni zinavyo pata faida bila kujali watendaji wake kistahiki.

Hata hivyo, Rais Biden amekuwa mwangalifu wa kutosema hadharani ni madai gani kati ya yale wanayoyahitaji anayaunga mkono ama kwa kiwango gani anaunga mkono maandamano hayo ya wafanyakazi hao.

Ongea nao yazinduliwa na ujumbe muhimu kwa Vijana
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 27, 2023