Spika wa Bunge la Uganda, Anita Among ametangaza kuwa Rais Museveni ametia saini mswada wa kupinga mapenzi ya jinsia moja kuwa sheria huku Taifa la Marekani likipinga hatua hiyo.

Spika Among amesema, kama Bunge la Uganda wamejibu kilio cha wananchi wao kwa kutunga sheria kulinda utakatifu wa familia wakati Biden akisema inakuika haki za kibidadamu.

Mara baada ya tangazo hilo, Rais wa Marekani Joe Biden akaishutumu sheria hiyo na kusema pia inahatarisha maendeleo ya uchumi wa nchi hiyo, iliyoko mashariki mwa bara la Afrika.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Biden alisema “Ninaungana na watu duniani kote wakiwemo watu wengi wa Uganda katika kuitaka sheria hiyo ifutwe mara moja, hakuna mtu anayestahili kuishi kwa kuhofia maisha yake wakati wote ni makosa.”

Young Africans yaichimba mkwara USMA
Afrika Kusini waanzisha taratibu wamkamate Rais Puttin