Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta amepuuza maneno ya Gwiji wa Soka nchini England Gary Neville kwamba kiwango cha sasa cha kipa David Raya kitawagharimu katika mipango yao ya kubeba ubingwa msimu huu.

Raya amekuwa akifanya makosa alipombadili Aaron Ramsdale golini na mwishoni mwa juma lililopita alifanya kosa jingine na kuwaruhusu Chelsea kufunga kupitia Mykhaylo Mudryk.

Baada ya mchezo huo uliopigwa jijini London, Neville alizungumza wasiwasi wake juu ya kipa Raya hana uwezo wa kumudu presha ya kuchezea timu kubwa.

Lakini, Kocha Arteta amejibu na kusema: “Sijaona kitu kama hicho tangu Raya, sijaona” akiwa na maana kipa Raya hana presha.

“Kuna presha ya kuchezea timu kubwa. Ni lazima ushinde mechi na muda wote uwe kwenye kiwango cha juu karibu katika kila mechi. Lakini, tukiangalia nafasi kwa nafasi, mtasemaje kuhusu beki wa kushoto. Mtasemaje kuhusu kiungo wa kati.

“Hivi mmeshauliza kuhusu Jorginho, Gabriel Jesus naye pia anaweza kuingia kwenye mjadala. Huo ndiyo uzuri wa mchezo huu. Makosa ni sehemu ya mchezo wa soka na makosa yamekuwa yakifanyika kwenye sehemu zote, mabeki, washambuliaji hadi kipa.”

Katika mchezo wa Mzunguuko watatu wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya uliopigwa usiku wa kuamkia leo dhidiya Sevilla iliyokuwa nyumbani, Raya alikuwa sehemu ya kikosi cha Arsenal kilichoibuka na ushindi wa 2-1.

Hat trick ya Aziz Ki yawaibua Simba SC
Ahmed Ally: Tumeionesha Afrika Simba ni nani