Watu wenye Silaha wanaosadikika ni wa Magenge ya Uhalifu, wamewauwa Wanafunzi 13 wa Shule ya Msingi ya Kiislamu wakati wa hafla ya kusherekea kuzaliwa kwa Mtume Mohammed, katika jimbo la kaskazini magharibi la Katsina la Nchini Nigeria.

Tukio hilo, limetokea eneo hilo ambalo ni kati ya maeneo ambayo yamekuwa yakikumbwa na mashambulizi ya magenge ya uhalifu ya majambazi, ambao huvamia Vijiji, kuua na kuteka nyara na kuchoma nyumba za Wananchi baada ya kufanya uporaji.

Magenge hayo, ambayo yana ngome katika misitu mikubwa inayozunguka majimbo ya Zamfara, Katsina, Kaduna na Niger, yamekuwa mashuhuri kwa matukio ya mara kwa mara ya utekaji nyara wa wanafunzi wa Shule katika miaka ya hivi karibuni.

Aidha, Kiongozi wa Wilaya ya Musawa, Habibu Abdulkadir amesema pia Watu wenye silaha waliokuwa kwenye Pikipiki walishambulia Kijiji cha Kusa cha Wilayani Musawa nyakati za usiku na kuwafyatulia risasi watoto wa shule waliokuwa wakisherekea Maulidi katika kijiji hicho.

Wizara, Wadau wakutana kujadili maboresho sekta ya Afya
Arsenal yajuta kumsajili Kai Havertz