Mamia ya Wafanyakazi wa mradi wa Reli ya kisasa – SGR, kambi ya Ihumwa Mkoani Dodoma, wameandamana kumshinikiza muajiri wao (YAPI MERKEZI), kuwalipa mafao yao wanayodai kwa kipindi chote cha kazi, baada ya kuondolewa kazini.

Hatua hiyo, inafuatia tangazo la Kampuni hiyo la kupunguza Wafanyakazi kutokana na uhaba ya kazi, huku ikidaiwa kuwa wapo hapo kwa siku kumi sasa wakipambania haki yao, ili waweze kuondoka eneo hilo.

Wanasema hali hiyo imewaathiri kwa kiasi kikubwa na wanashindwa kuendelea na maisha yao ya kawaida na kwamba baadhi yao wamekuwa wakiishi mitaani na kwamba wanaamini njia waliyoitumia kudai stahiki zao ni sahihi

Mbali na usafirishaji wa mizigo na Watu, SGR pia itachochea maendeleo ya sekta zingine za kiuchumi kama Kilimo, Viwanda na Biashara katika mikoa inapopita Reli hiyo na Nchi jirani ikiwemo Kenya, DRC, Uganda, Burundi na Rwanda.

Kenya: 70 wafariki kwa El-nino, Rais aitisha mkutano wa dharula
Rais anataka mahusiano mazuri Wafanyabiashara, TRA - Dkt. Biteko